KINSHASA:Mbeki afanya ziara ya kikazi Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo | Habari za Ulimwengu | DW | 21.08.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

KINSHASA:Mbeki afanya ziara ya kikazi Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo

Rais Thabo Mbeki wa Afrika Kusini amewasili nchini Jamhuri ya kidemokrasi ya Kongo kufanya ziara ya kikazi nchini humo yenye lengo la kuinua kiwango cha uhusiano baina ya nchi mbili hizo.

Rais Mbeki na wenyeji wake wanatarajiwa kutathimini ushirikiano wao katika masuala ya usalama,uchumi,fedha na katika miradi ya maendeleo.

Rais Mbeki anafanya ziara hiyo muda mfupi baada ya rais J. Kabila wa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo kuitembelea Afrika Kusini mnamo mwezi juni.

Matangazo

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com