Kimbunga chauwa zaidi ya watu 150 Ufilipino | Matukio ya Kisiasa | DW | 22.06.2008
 1. Inhalt
 2. Navigation
 3. Weitere Inhalte
 4. Metanavigation
 5. Suche
 6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Matukio ya Kisiasa

Kimbunga chauwa zaidi ya watu 150 Ufilipino

Kimbunga kikali kimeendelea kuipiga Ufilipino kwa siku ya pili leo hii na kuuwa takriban watu 155,wengine zaidi ya 800 bado hawajulikani walipo wakati wakiwa ndani ya kivuko inachoripotiwa kuwa kinazama .

Wakaazi wakiwa kwenye mtaa wa Manila uliofurika kutokana na mvua kubwa zilizosababishwa na kimbunga Fengshen Jumapili ya tarehe 22 mwezi wa Juni mwaka 2008.

Wakaazi wakiwa kwenye mtaa wa Manila uliofurika kutokana na mvua kubwa zilizosababishwa na kimbunga Fengshen Jumapili ya tarehe 22 mwezi wa Juni mwaka 2008.

Kimbunga hicho pia kimewapotezea makaazi wengine maelfu kutokana na mafuriko na maporomoko ya ardhi.

Watu 59 wameuwawa katika jimbo la kati la Iloilo lilioko kilomita 560 kusini mwa mji mkuu wa Manila ambapo miji kadhaa imefurikwa na maji wakati kimbunga hicho Fengshen kilipopiga kwanza eneo hilo hapo jana.

Gavana wa Iloilo Neil Tupas ametangaza jimbo hilo kuwa katika hali ya maafa wakati akielezea hofu yake kwamba idadi ya vifo inaweza kupindukia watu 100 kutokana na maeneo mengi kuwa hayawezi kufikiwa.

Kimbunga hicho kimesababisha mvua mkubwa na upepo mkali unaosafiri kilomita 120 kwa saa ambao pia umekata nguvu za umeme na kusababisha uharibifu mkubwa sana kwa majengo.

 • Tarehe 22.06.2008
 • Mwandishi Mohamed Dahman
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo https://p.dw.com/p/EOFs
 • Tarehe 22.06.2008
 • Mwandishi Mohamed Dahman
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo https://p.dw.com/p/EOFs
Matangazo

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com