1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MigogoroKorea Kaskazini

Kim Jong Un ajivunia mafanikio ya jeshi la nchi yake

12 Desemba 2025

Kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong Un amesifu mafanikio ya nchi yake mwaka 2025, ikiwa ni pamoja na kutuma wanajeshi kwenye operesheni za kijeshi nje ya mipaka ya nchi hiyo.

https://p.dw.com/p/55CIf
Korea Kaskazini | Jeshi
Wanajeshi wa Korea Kaskazini wakishika doria katika mto Yalu karibu na mji wa SinuijuPicha: Wu Hong/EPA/picture alliance

Kim amekuwa akiongoza mikutano muhimu wiki hii ili kujadili mipango ya sera na namna ya kuitekeleza, wakati nchi hiyo inapojiandaa kwa mkutano wa tisa wa chama cha Wafanyakazi cha Korea, unaotarajiwa kufanyika mapema mwaka ujao.

Shirika la Habari la serikali KCNA limeripoti kuwa, kiongozi huyo ameeleza umuhimu wa Korea Kaskazini kujitegemea zaidi na kuongeza kasi ya maendeleo ya kiuchumi na kijamii.

Katika hatua nyingine, Kim Jong Un na Rais wa Urusi Vladimir Putin wamesaini mkataba wa pamoja wa ulinzi huku Korea Kaskazini ikiripotiwa kutuma wanajeshi wake katika uwanja wa vita kuisaidia Urusi katika vita vyake dhidi ya Ukraine.

Inaripotiwa kuwa Korea Kaskazini inapokea msaada wa kifedha, teknolojia ya kijeshi, pamoja na nishati kutoka Moscow kama malipo kwa hatua yake kutuma wanajeshi kuisaidia Urusi.