1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

KHARTOUM: Sudan yakubali kikosi cha kulinda amani kipelekwe Darfur

18 Juni 2007
https://p.dw.com/p/CBqh

Wajumbe wa serikali ya Sudan na wajumbe wa baraza la usalama la Umoja wa Mataifa wamethibitisha kuwa serikali ya mjini Khartoum imekubali bila masharti kikosi cha kulinda amani Darfur kitakachojumulisha wanajeshi wa Umoja wa Mataifa na Umoja wa Afrika.

Tangazo hilo lilitolewa kufuatia mazungumzo kati ya wanachama wa baraza la usalama la Umoja wa Mataifa na rais wa Sudan, Omar Hassan al Bashir, juu ya kikosi hicho cha pamoja.

Tume ya kulinda amani Darfur itajumulisha wanajeshi 19,000 watakaopelekwa katika eneo la magahribi mwa Sudan.

Sudan ilikubali kikosi hicho juma lililopita lakini haijabainika wazi kikosi hicho kitaongozwa na nani.