Kesi ya Taylor yaendelea. | Habari za Ulimwengu | DW | 08.01.2008
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

Kesi ya Taylor yaendelea.

The Hague.

Kesi ya uhalifu wa kivita inayomkabili rais wa zamani wa Liberia Charles Taylor inaendelea mjini The Hague leo. Taylor anatuhumiwa kwa kuwaongoza majeshi ya waasi katika nchi jirani ya Sierra Leone, ambao walifanya uhalifu wa kuwakata watu viungo, kama miguu na mikono wakati wa vita vya miaka kumi vya wenyewe kwa wenyewe nchini humo.

Amekana madai hayo yote dhidi yake. Mahakama hiyo inayoungwa mkono na umoja wa mataifa kwa ajili ya Sierra Leone ilihamishwa kutoka taifa hilo la Afrika magharibi na kwenda The Hague kwa sababu za kiusalama ili kuwahukumu wale waliohusika katika vita vya mwaka 1991 – 2002.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com