Kesi ya Radovan Karadzic | Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili | DW | 02.03.2010
 1. Inhalt
 2. Navigation
 3. Weitere Inhalte
 4. Metanavigation
 5. Suche
 6. Choose from 30 Languages

Timu Yetu

Kesi ya Radovan Karadzic

Karadzic amevielezea vita vya miaka ya 1990 kama vita vitakatifu

default

Kiongozi wa zamani wa Waserbia wa Bosnia, Radovan Karadzic.

Kiongozi wa zamani wa Waserbia wa Bosnia, Radovan Karadzic amevielezea vita vya Bosnia vya miaka ya 1990, kama vita vitakatifu vilivyofanywa na Waserbia dhidi ya Waislamu waliokuwa wanataka kuigeuza Bosnia kuwa jamhuri ya Kiislamu.

Kauli hiyo ameitoa jana katika mahakama ya kimataifa ya The Hague na alidai kuwa analitetea taifa lake na sio yeye mwenyewe. Karadzic ameiambia mahakama hiyo kuwa uongozi wa Kiislamu wa Bosnia kwa wakati huo ulikua na hatia ya kuanzisha uadui kwa kukataa mpango wa kugawana madaraka.

Ameongeza kuwa kila kitu kilichofanywa na Waserbia kama sehemu ya kujitetea kwao mahakama ya Umoja wa Mataifa inakichukulia kama kosa la uhalifu. Karadzic hana wakili na anajitetea mwenyewe katika mahakama hiyo iliyopo nchini Uholanzi.

 • Tarehe 02.03.2010
 • Mwandishi Kabogo Grace Patricia
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo https://p.dw.com/p/MHK1
 • Tarehe 02.03.2010
 • Mwandishi Kabogo Grace Patricia
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo https://p.dw.com/p/MHK1
Matangazo

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com