Kesi ya maafa ya Duisburg yaanza
27 Julai 2010Kulingana na msemaji wa afisi ya mwendesha mashtaka,mahakama itatathmini mbinu zilizotumika kuwaruhusu watu zaidi ya milioni moja kushiriki katika tamasha hilo kinyume na idadi ya laki mbili u nusu iliyokubaliwa.
Idadi ya waliouawa wakati msongamano ulipotokea inaripotiwa kuongezeka na imefikia 20 kwa sasa nayo malalamiko yanawaandama waandalizi wa tamasha hilo.
Tamasha hilo limekuwa likifanyika katika mji mkuu wa Berlin hadi mwaka 2006 lilipoanza kuhamishiwa miji tofauti ya Ujerumani.Tamasha la mwaka uliopita lilipangwa kufanyika mjini Bochum ila likafutwa kwasababu za kiusalama.Kulingana na muandalizi wa shughuli hiyo,Rainer Schaller,ili kuonyesha heshima kwa waliopoteza maisha yao,tamasha hilo halitowahi kufanyika tena