Kesi ya Demjanjuk | Matukio ya Kisiasa | DW | 12.05.2009
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Matukio ya Kisiasa

Kesi ya Demjanjuk

Mlinzi wa kambi ya Manazi kukabili Mashtaka Ujerumani.

Ndege iliomlegta Demjanjuk Munich.

Ndege iliomlegta Demjanjuk Munich.

Baada ya vuta nkuvute ya muda mrefu ,mtuhumiwa uhalifu enzi za utawala wa Manazi "Iwan the Terrible" -John Demjanjuk, Marekani ilimkabidhi leo Ujerumani.Katika gereza karibu na Munich,mzee huyo mwenye umri wa miaka 89 amepangiwa kusomewa waranti wa kutiwa nguvuni.

Sobibor -Poland iliokaliwa na Ujerumani, ndiko ilipokuwa kambi ya manazi ya kuwahilikisha mayahudi.Hadi binadamu 2000 wakiuliwa kila siku katika vyumba vya gesi.Kwa jumla, inakisiwa mayahudi 250.000 walihilikishwa humo.

Walinzi wa kambi hiyo wakiwapakia wahanga wao ndani ya magari-moshi hadi kwenye vyumba hivyo vya gesi.Halafu wakiwazika maiti katika makaburi ya umma wa watu na baadae wakisafisha vyumba hivyo vya gesi tayari kwa kundi jengine.

Mmoja kati ya walinzi hao waliosaidia kuwahilikishja mayahudi hao atuhumiwa kuwa mzaliwa wa Ukraine .John Demjanjuk.Yasemekana baina ya mwezi machi na septemba, 1943 alishiriki katika kuwahilikisha hadi mayahudi 29,000.Alitimniza kazi hiyo akisaidiwa na wasaidizi wa kujitolea waliofunzwa kaszi hiyo katika kambi ya mafunzo ya M anazi.Hii ni kwa muujibu wa nyaraka zinavyoonesha.

Kwamba Demjanjuk alikuwa mateka na mfungwa wa Ujerumani ya Manazi na alijitolea kufanya kazi hiyo kwa kuhofia maisha yake ,hali hiyo haipunguzi hatia yake.Hatahivyo, Demjanjuk anakanusha tuhuma hizo zote na anasema, hakujua kile kilichokua kikipita katika kambi ya Sobibor na baadae ile ya Majdanek na Flossenburg.Binafsi, anadai alikuwa mfungwa wa vita.Lakini kwa jicho la ushahidi uliopo na kutokana na ujuzi wa kihistoria ,madai yake hayaaminiki sana.Kwani, Demjanjuk alikuwa mzungushaji gurudumu la kiwanda cha mauaji....

Kwa kesi yake mjini Munich ,inaanza mojawapo ya kesi za mwisho za Manazi nchini Ujerumani.Ni kesi dhidi ya mzee aliefikisha sasa umri wa miaka 89 na pengine mgonjwa. ...

Demjanjuk anapewa mashtaka ya kisheria ambayo yanazingatia umri na afya yake .Bila ya shaka, kesi yake itakuwa ngumu,itakayozorota muda mrefu na matokeo yake hayajulikani.Taabu itakuwa kumtwika pekee mabegani mwake jukumu la yaliopita na ushahidi wake. Kwahivyo, je, kesi hii hafai kuendeshwa ? La, hasha.

Iwapo Demjanjuk ataishia gerezabni Ujerumani ni jambo linalotiliwa shaka shaka kubwa.Mahkama za Ujerumani baada ya kupita zaidi ya miongo 6 tangu kumalizika utawala wa vitiosho wa manazi, zinaweka wazi kuwa: hakuna yeyote alieusaidia utawala wa manazi kuhilikisha wenzake au alieutumikia,afaa leo kusamehewa.Umri pekee hauutoshi kukwepa hatia. Kesi mjini munich pżia ni dalili ya kusikizwa malalamiko dhidi ya unyama na ushenzi uliopita.

muhimu zaidi ni ishara inayokwenda kwa wale walionusurika kuhilikishwa na kwa jamaa zao :Kesi hii, ni kutumikia ukweli,haki na utu bila kutegemea iwapo mwishoe, Demjanjuk atapitishiwa adhabu yoyote....

Mtayarishaji:Ramadhan Ali

Mhariri: Muhammed Abdul Rahman

Matangazo

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com