Kansa huathiri watoto walio karibu na mitambo ya nuklea | Habari za Ulimwengu | DW | 08.12.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

Kansa huathiri watoto walio karibu na mitambo ya nuklea

BERLIN

Utafiti wa serikali ya Ujerumani umegunduwa kwamba watoto wanaoishi karibu na mitambo ya kuzalisha umeme kwa nguvu za nuklea wako rahisi zaidi kupata ugonjwa wa kansa ya damu au wa kans a ya mifupa.

Ujerumani hivi sasa ina mitambo 16 ya kuzalisha umeme kwa nguvu za nuklea ambayo yote inatazamiwa kufungwa ifikapo mwaka 2022.Utafiti huo uliofanywa na Mrajisi wa Kansa ya Watoto nchini Ujerumani umesema kwamba watoto 37 wanaoishi umbali usiozidi kilomita 5 kutoka mitambo hiyo wamekuja kuathirika na kans a ya damu katika kipindi kati ya mwaka 1980 na mwaka 2003.

Wastani wa takwimu nchini Ujerumani ungeliweza kutabiri kesi 17 katika kundi hilo la watoto.

Waziri wa Mazingira wa Ujerumani Sigmar Gabriel amesema kamati ya serikali ya viwango vya usalama vya sumu ya miale ya nuklea itachanganuwa utafti huo.

Matangazo

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com