Kanda ya video yamuonyesha Mjerumani alietekwa nyara
19 Agosti 2007Matangazo
Katika kanda hiyo ya video,mfanyakazi huyo wa shirika la Kijerumani linalotoa misaada,“ora international“ ametaja jina lake na kuonyesha kitambulisho chake cha Kijerumani.Mfanyakazi huyo alie na miaka 31 alitekwa nyara katika mkahawa mjini Kabul.
Tume ya dharura iliyoundwa na Wizara ya Mambo ya Nje ya Ujerumani inafanya bidii ili mfanyakazi huyo apate kuachiliwa huru.Kwa mujibu wa polisi wa Afghanistan,Mjerumani huyo hakutekwa nyara na wanamgambo wa Taliban,bali ni kundi la majambazi lililohusika na uhalifu huo.