KABUL: Operesheni ya kijeshi Afghanistan imeua Wataliban 15
15 Julai 2007Matangazo
Wanamgambo 15 wa Kitaliban wameuawa kusini mwa Afghanistan katika operesheni iliyofanywa kwa pamoja na majeshi ya Afghanistan na Kanada.Hayo ni kwa mujibu wa majeshi yanayoongozwa na NATO nchini Afghanistan.Wakati huo huo Waafghanistan 6 waliokuwa wakifanyia kazi kampuni la kigeni linalotoa ulinzi,wameuawa mashariki mwa nchi.Watu hao walikuwa ndani ya gari,katika wilaya ya Paktika,bomu liliporipuliwa.