Kabul. Majeshi ya muungano yadai kumuua mshirika wake Osama. | Habari za Ulimwengu | DW | 23.12.2006
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

Kabul. Majeshi ya muungano yadai kumuua mshirika wake Osama.

Jeshi la Marekani nchini Afghanistan limesema kuwa majeshi ya muungano yamemuua mshirika wa karibu wa Osama bin Laden. Jeshi limesema kuwa Mullah Akhtar Mohammed Osman pamoja na wapiganaji wengine wawili wameuwawa katika shambulio la anga kusini mwa Afghanistan.

Osman ni mmoja kati ya viongozi wanne wa juu wa kundi la Taliban, na alikuwa akiongoza mapigano kusini mwa nchi hiyo.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com