Kabul. Kikosi cha polisi tisa chalipuliwa kwa bomu.
13 Machi 2007Matangazo
Kiasi cha polisi tisa wameuwawa katika bomu lililolipuliwa kwa mbali katika jimbo la magharibi la Farah nchini Afghanistan.
Maafisa wa usalama wamesema kuwa gari ya polisi ilikanyaga bomu hilo lililokuwa limetegwa kando ya barabara wakati wakisafiri katika barabara kuu katika jimbo hilo.
Miongoni mwa waliouwawa ni pamoja na kamanda wa polisi wa jimbo hilo.
Hakuna kundi lililodai mara moja kuhusika na shambulio hilo.