Jinsi ya kuwaandama wakwepa kodi | Magazetini | DW | 02.02.2010
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Magazetini

Jinsi ya kuwaandama wakwepa kodi

Yafaa kununua taarifa kinyume na sheria ?

Angela Merkel

Angela Merkel

Maoni ya wahariri wa magazeti ya Ujerumani leo , yamechambua mada mbali mbali. Usoni kabisa ni jinsi gani kupambana na wanaokwepa kulipa kodi na kuficha fedha zao katika mabenki ya Uswisi.

Bajeti alioitangaza Rais Barack Obama wa Marekani, pamoja na kusimamishwa mradi wa misafara ya anga za juu ya shirika la NASA, ni mada nyengine iliochambuliwa.

Gazeti la Rhein-Neckar-Zeitung laandika:

"Katika mkasa wa serikali ya Ujerumani kununua kinyume na sheria taarifa za banki, yafaa kufuata kanuni ya kuitumia fursa ilioibuka.Na hakuna wakati huu muhimu zaidi kwa Kanzela Merkel ambae wiki hii ametimiza kipindi kisicho pendeza cha siku 100 madarakani (tangu ucahguizi ) kuliko kufuata mkondo wa maoni ya wananchi.Na hata hii , inafahamika:Ikiwa serikali inadai kutoka wanyonge wanaolipwa ruzuku ya (Hartz IV ) warudishe Euro 20 tu za nyongeza ya ruzuku za watoto wao,basi haiwezi kuwafumbia macho wale waliokwepa kulipa kodi kwa serikali."

Ama gazeti la BILDZEITUNG linalochapishwa Berlin linakumbusha kwamba, kukwepa kulipa kodi Ujerumani, ni uhalifu.Yule ambae anaihadaa Idara ya kodi,atazamie kupigwa faini na hata kutiwa korokoroni.

Gazeti linaongeza:

"Hayo wanaelewa vizuri majambazi hao wanaoihadaa serikali na kutorosha kisirisiri fedha zao hadi Uswisi. ...Serikali yapaswa kutumia kila mbinu kuwakamata .Kwani, ina jukumu la kufanya hivyo kwa walipa kodi.Ikiwa hii itawezekana kwa msaada wa taarifa za mabenki zilizoibiwa,fursa hiyo pia itumiwe.Kwani, hapa wamehusika majambzi 1.500 na si kidogo.Ni sawa na haraka Kanzela Merkel kuamua kununua taarifa hizo. Yachekesha kuona wanaopaza sauti kulalamika , ni wale wale waliowakaribisha nyumbani mwao majambazi hao wasiolipa kodi.Salamu inazotoa serikali ya Ujerumani, ni hizi:Anaekwepa kulipa kodi,atakiona kilichomtoa kanga manyoya."

Likitugeuzia mada ,gazeti la Trierischer Volksfreund, linaichambua bajeti ya serikali ya rais Obama wa Marekani:Gazeti laandika kwamba, kutoka mtu aliewekewa matumaini kuikomboa Marekani baada ya miaka 8 ya utawala wa George Bush ,sasa amegeuka rais wa madeni makubwa rahisi kukosolewa. Volksfreund laongeza:

"Marekani ikiwa na kasoro kubwa katika bajeti yake ambayo haikuwahi kuonekana tangu kumalizika vita vya pili vya dunia na bajeti ya kubana matumizi,rais Obama anakipa chambo chama cha upinzani kumshambulia mwaka huu wa uchaguzi wa Bunge la Kongress. Kwa tarakimu zilizotolewa jana mjini Washington, kuna mambo mawili yasiofurahisha:Rais huyu mpya ameteleza sana kutoka ile hali ya fedha aliyoibashiri itavyokuwa pamoja na mpango wake wa kustawisha uchumi alioutangaza muda mfupi baada ya kuapishwa.Mpango huo haukutimiza shabaha yake ya kutoa nafasi za kazi."

Mwandishi: Ramadhan Ali /DPA

Uhariri: Abdul-Rahman