ISLAMABAD:Rais Musharaf asema apenda ′′Demokrasia′′hawezi kutangaza hali ya hatari | Habari za Ulimwengu | DW | 09.08.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

ISLAMABAD:Rais Musharaf asema apenda ''Demokrasia''hawezi kutangaza hali ya hatari

Rais wa Pakistan hakutangaza hali ya hatari kama ilivyotarajiwa kufuatia uvumi uliokuwa umejitokeaza awali nchini Pakistan.

Msemaji wa serikali amesema rais Musharraf alikuwa akikabiliwa na shinikizo za kumtaka tangauze hali ya hatari lakini alifikia uamuzi wa kutofanya hivyo kwasababu anaunga mkono Demokrasia. Ripoti za awali zilisema kuwa serikali ilikuwa ikijadiliana juu ya kutangaza hali ya hatari kutokana na vitisho kutoka nje na ndani ya nchi.Baadhi ya wapinzani na watu mashuhuri nchini Pakistan wameitafsiri dhana na kutaka kutangazwa hali ya hatari kama njia iliyotaka kutumiwa na Rais Musharaf kujirefushia muda wa uongozi . Endapo hali ya hatari ingetangazwa bwana Musharaf angeweza kuhairisha uchaguzi mkuu utakaofanyika baadae mwakani ambapo angeweza kujirefushia kipindi cha uongozi.

Matangazo

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com