ISLAMABAD:Jaji mkuu aendelea kupambana na rais Musharraf nchini Pakistan | Habari za Ulimwengu | DW | 05.05.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

ISLAMABAD:Jaji mkuu aendelea kupambana na rais Musharraf nchini Pakistan

Jaji mkuu aliefukuzwa kazi nchini Pakistan bwana Iftikhar Mohammed Choudry leo ameenda katika mji wa Lahore mashariki mwa nchi hiyo ili kuwahutubia watu wanaomwuunga mkono katika mapambano yake dhidi ya rais Pervez Musharraf aliemfukza kazi jaji mkuu huyo kwa madai kwamba alikuwa anatumia vibaya wadhifa wake.

Maandamano makubwa yamefanyika kumwuunga mkono jaji mkuu huyo tokea rais Musharraf alipochukua hatua ya kumkataza kufanya kazi kama jaji mkuu.

Bwana Choudry anatarajiwa kuwahutubia wanasheria na watu wengine wanaomwuunga mkono katika mji wa Lahore.

Matangazo

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com