ISLAMABAD: Rais Musharraf ameahidi kuacha madaraka ya kijeshi
12 Novemba 2007Matangazo
Rais wa kijeshi wa Pakistan,Jemadari Pervez Musharraf ametetea uamuzi wake wa kutangaza hali ya hatari.Alipozungumza na waandishi wa habari mjini Islamabad,Musharraf vile vile aliahidi kujiuzulu jeshini na kuapishwa kama rais pale Mahakama Kuu itakapoidhinisha hatua iliyomchagua kuendelea na wadhifa huo.Kiongozi huyo wa kijeshi akaongezea,uchaguzi mkuu unapaswa kufanywa kabla ya tarehe 9 Januari lakini hakutaja tarehe ya kuondosha hali ya hatari.