1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Iran yatishia kushambulia miundo mbinu ya nishati

23 Machi 2026

Tamko la Iran la kutishia kushambulia miundo mbinu ya nishati ya mataifa ya ghuba limefuatia kauli ya rais Donald Trump ya kutishia kushambulia mitambo muhimu ya nishati ya Iran

https://p.dw.com/p/5Augh
Trump ametowa muda wa saa 48 tangu Jumamosi (20.03.2026) kwa Iran kufunguwa mlango bahari wa Hormuz
Trump ametowa muda wa saa 48 tangu Jumamosi (20.03.2026) kwa Iran kufunguwa mlango bahari wa HormuzPicha: Cn-str/AFP/Getty Images

Kiongozi wa kamandi kuu ya jeshi la Marekani Brad Cooper amesema kampeini ya kijeshi dhidi ya Iran iko kwenye mpango katika wakati jeshi la Israel limeanza kile imekiita wimbi kubwa la mashambulizi yanayolenga miundo mbinu ya utawala wa Tehran, leo Jumatatu.

Mashambulizi hayo yanafanywa baada ya Tehran kuonya huenda ikashambulia miundo mbinu ya nishati katika mataifa ya ghuba na maslahi ya Marekani na Israel  ikiwa mataifa hayo yatajaribu kuendelea kutekeleza kitisho cha rais Donald Trump.Marekani na Iran zatishia kushambulia miundombinu muhimu

Kiongozi huyo wa Marekani ametishia kushambulia mitambo ya nishati ya Iran ikiwa Tehran haitofunguwa kikamilifu mlango bahari wa Hormuz ndani ya kipindi cha saa 48.

Idadi ya waliouwawa kufuatia vita hivyo vya mashariki ya kati ni zaidi ya watu 1500 nchini Iran, zaidi ya 1,000 Lebanon,15 nchini Israel na wanajeshi 13 wa Marekani na raia kadhaa katika mataifa ya ghuba. Mamilioni ya raia wameachwa bila makaazi Lebanon na Iran.