1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Iran kuwazuia wakaguzi wa IAEA katika vinu vyake

John Juma
15 Februari 2021

https://p.dw.com/p/3pNwt

Iran imesema itazuia uchunguzi wa mapema wa shirika la Umoja wa Mataifa la kudhibiti nishati ya atomiki, IAEA kuanzia wiki ijayo, ikiwa wahusika wengine kwenye mkataba wa nyuklia wa Iran hawatatimiza ahadi zao. Hatua hiyo inaleta changamoto kwa matumaini ya rais wa Marekani Joe Biden kuufufua mkataba huo. John Juma amezungumza na mchambuzi wa masuala ya kimataifa Ahmed Rajab akiwa London kuhusu lengo hilo la Iran.