Idadi ya watu waliokufa kwa kipindupindu Haiti yaongezeka | Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili | DW | 25.10.2010
 1. Inhalt
 2. Navigation
 3. Weitere Inhalte
 4. Metanavigation
 5. Suche
 6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Timu Yetu

Idadi ya watu waliokufa kwa kipindupindu Haiti yaongezeka

Imeelezwa kuwa idadi ya watu waliokufa kwa ugonjwa wa kipindupindu nchini Haiti imefikia 250, huku wengine 3,000 wakiwa wameambukizwa ugonjwa huo.

Wagonjwa wa kipindupindu wakisubiri huduma katika hospitali moja nchini Haiti.

Wagonjwa wa kipindupindu wakisubiri huduma katika hospitali moja nchini Haiti.

Idadi wa watu waliokufa kutokana na ugonjwa wa kipindupindu nchini Haiti imefikia 250, huku wengine 3,000 wakiwa wameambukizwa ugonjwa huo.

Watu watano wameambukizwa ugonjwa huo kwenye mji mkuu wa nchi hiyo, Port-au-Prince, lakini maafisa wa Umoja wa Mataifa wamesema wagonjwa hao waligundulika haraka na hatimaye kutengwa.

Mkurugenzi Mkuu katika wizara ya afya nchini Haiti, Gabriel Thimote, amesema ana matumaini kuwa ugonjwa huo unaweza ukadhibitiwa. Thimote amesema hali inaonekana kuimarika, ingawa ugonjwa huo huenda ukafikia katika kiwango cha juu.

Wafanyakazi wa afya wamekuwa wakikabiliana na ugonjwa huo mjini Port-au-Prince nje ya kambi wanakoishi zaidi ya watu milioni moja walioathiriwa na tetemeko la ardhi lililotokea mwezi Januari, mwaka huu.

Shirika la msaada la Oxfam linagawa dawa za kuweka kwenye maji, pakiti za dawa za kuongeza nguvu mwilini na vipande vya sabuni kwa zaidi ya watu 25,000.

 • Tarehe 25.10.2010
 • Mwandishi Kabogo Grace Patricia
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo https://p.dw.com/p/Pmfx
 • Tarehe 25.10.2010
 • Mwandishi Kabogo Grace Patricia
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo https://p.dw.com/p/Pmfx
Matangazo

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com