Idadi ya waliofariki Duisburg yafikia 21 | Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili | DW | 29.07.2010
 1. Inhalt
 2. Navigation
 3. Weitere Inhalte
 4. Metanavigation
 5. Suche
 6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Timu Yetu

Idadi ya waliofariki Duisburg yafikia 21

Idadi ya waliopoteza maisha yao katika msongamano kwenye tamasha la Love-parade la wikendi imefikia 21.

Purukushani zilizotokea kwenye tamasha la Loveparade

Purukushani zilizotokea kwenye tamasha la Loveparade

Kulingana na maafisa wa serikali,mwanamke mmoja aliye na umri wa miaka 25 amefariki kwasababu ya majeraha aliyoyapata wakati wa purukushani hizo zilizotokea mwishoni mwa wiki iliyopita.Ziadi ya watu 500 walijeruhiwa.Waziri wa mambo ya ndani wa Mkoa wa North-Rhein Westphalia ,Ralf Jäger amewalaumu waandaji wa tamasha hilo kwa kutowajibika.

Kulingana na kiongozi huyo,lango kuu la eneo la tamasha lilifunguliwa kuchelewa jambo lililosababisha msongamano.Takwimu za polisi zinaonyesha kuwa kiasi cha watu laki nne walikuwako kwenye eneo la tukio.Ibada maalum ya ukumbusho imepangwa kufanyika mjini Duisburg ifikapo Jumamosi.Rais wa Ujerumani Christian Wulff na Kansela Angela Merkel wanatarajiwa kuhudhuria shughuli hiyo.

p> Eneo lilikuwa dogo
NO FLASH Loveparade Massenpanik Duisburg Absperrung Gitter

Eneo la mkasa wa mwishoni mwa wiki iliyopita,Duisburg

Kwa sasa wachunguzi wanayatathmini mazingira yaliyosababisha maafa hayo ambayo huenda yalichangiwa na kutowajibika.Kulingana na Mwendesha mashtaka mkuu wa mji wa Duisburg,Rolf Haferkamp,mahakama itaichunguza mipango ya usalama iliyoandaliwa pamoja na idadi ya waliohudhuria tamasha iliyopindukia.Bwana Haferkamp alifafanua kuwa uchunguzi huo huenda ukachukua muda wa wiki kadhaa au hata miezi.

Uongozi wa mji huo pamoja na waandalizi wamekosolewa kwa kuruhusu idadi kubwa ya watu kuingia katika eneo dogo kulikofanyika tamasha lenyewe.Kiasi cha watu milioni 1.4 wanaripotiwa kukusanyika kwenye eneo hilo la tukio kinyume na idadi iliyoruhusiwa ya alfu 250.Wakati yote hayo yakiendelea,tetesi zimejitokeza kuwa uongozi wa mji uliziupuuza kauli maafisa wa polisi za kutoliandaa tamasha hilo la muziki wa Rock mjini humo kwasababu za kiusalama.Katika taarifa yake,Meya wa Duisburg Adolf Sauerland,alisema iwapo uongozi wa mji haukuwajibika,basi utachukua dhamana.

Uchunguzi kamili

Kwa sasa Meya huyo wa Duisburg ameusisitizia umuhimu wakufanya uchunguzi kamili kwanza hata anapoandamwa na madai ya kumtaka ajiuzulu.

Mkasa huo wa Jumamosi ulitokea karibu na lango la pekee la kuingia kwenye uwanja wa tamasha.Takwimu za polisi zinaonyesha kuwa watu zaidi ya 500 walijeruhiwa.Imebainika kuwa hilolimechangia pakubwa katika mkasa huo.Kwa mujibu wa mtaalam mmoja wa usalama anayesimamia kampuni moja ya inayotoa huduma za usalama kwenye matamasha,lilikuwa jambo la kushangaza kwa uongozi wa mji kuidhinisha kibali cha kuandaa shughuli hiyo.

Flash-Galerie Loveparade Duisburg 2010

Shamrashamra kabla ya mkasa kutokea

Kuna tetesi kuwa uongozi wa mji uliupuuza wito wa maafisa wa polisi wa kutowapa vibali waandalizi wa tamasha hilo ambalo ni moja ya matamasha makubwa ya muziki aina ya Rock kwasababu mji wa Duisburg haukuwa na uwezo wa kupambana na dharura ya aina hiyo.7 kati ya watu hao waliofariki wanaripotiwa kutokea mataifa ya Austria,Italia,Uholanzi,China,Bosnia na Uhispania.

Masuali yote hayo yameulizwa na hata Waziri Mkuu wa jimbo la North-Rhein Westphalia Hannelore Kraft amesema kuwa mipango ya usalama haikuwa imeandaliwa vizuri.

Tamasha la Loveparade lilianzia katika mji mkuu wa Berlin ulio na jumla ya wakazi milioni 3.4 na mwaka 2006 lilifanyika kwenye uwanja mkubwa.Mji wa Duisburg una jumla ya wakazi laki 5.

Mwaka uliopita uongozi wa mji wa Bochum ulilazimika kulifuta tamasha hilo kwasababu za kiusalama zilizotolewa na polisi wa eneo hilo.

 • Tarehe 29.07.2010
 • Mwandishi Thelma Mwadzaya
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo https://p.dw.com/p/OX4T
 • Tarehe 29.07.2010
 • Mwandishi Thelma Mwadzaya
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo https://p.dw.com/p/OX4T
Matangazo

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com