Idadi ya vifo yaongezeka kufuatia mashambuilzi ya mabomu Pakistan | Habari za Ulimwengu | DW | 24.11.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

Idadi ya vifo yaongezeka kufuatia mashambuilzi ya mabomu Pakistan

Idadi ya vifo kutokana na mashambulizi mawili ya mabomu yaliyofanywa na watu wa kujitoa muhanga maisha dhidi ya wanajeshi katika mji wa Rawalpindi, kusini mwa mji mkuu Islamabad nchini Pakistan imefikia 20.

Motokaa ya kwanza ililigonga basi lililokuwa limewabeba wanajeshi katika jengo la wakala wa ujasusi na kuwaua watu 13.

Mshambuliaji wa pili alikishambulia kituo cha ukaguzi karibu na makao makuu ya jeshi la Pakistan, karibu kilomita tatu kutoka eneo lililoshambuliwa kwanza.

Mashambulizi hayo yanazidisha shinikizo dhidi ya rais Pervez Musharraf aondoe utawala wa haliy a hatari nchini Pakistan.

Hujuma hizo zimefanywa wakati waziri mkuu wa zamani, Nawaz Sharif, akitarajiwa kurejea nchini humo kutoka uhamishoni nchini Saudi Arabia. Kurejea kwake huenda kukabadili hali ya kisiasa nchini Pakistan huku uchaguzi ambao upinzani umetishia kuugomea, ukikaribia kufanyika terehe 8 mwezi Januari mwakani.

Matangazo

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com