Hukumu ya Mahkama ya katiba | Magazetini | DW | 12.03.2008
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Magazetini

Hukumu ya Mahkama ya katiba

Mahkama kuu ya katiba huko Karlsruhe yazima sheria ya kusajili nambari za magari majiani.

Wolfgang Schaeuble

Wolfgang Schaeuble

Mada kuu iliochambuliwa na wahariri wa magazeti ya Ujerumani hii leo, ni hukumu ya Mahkama Kuu ya katiba kutoruhusu serikali tangu ya shirikisho hata zile za mikoa kusajili moja kwa moja zitakavyo nambari na alama za motokaa zinazosafiri barabarani.

Gazeti la OSTSEEZEITUNG linalochapishwa mjini Rostock laandika:

"Hukumu hiyo ya Mahkama Kuu ya Katiba ni ushindi kwa haki za raia juu ya matamanio ya polisi.Ni barabara kwa mahkama kuu ya karlrsruhe kuilinda katiba na hivyo kutulinda sisi raia na mkono wa mashtaka usio na kikomo.Taarifa ambazo polisi inazoweza kujipatia wazi wazi na itakavyo na hasa kwa serikali ambayo hupenda kudhibiti kila kitu huongoza katika hali kama hiyo kama ilivyokua katika ile iliokua Ujerumani mashariki (GDR) na idara yake ya usalama wa taifa-Stasi.

Ni vyema kwahivyo,katika kuamia jinsi gani na inamhusu nani na lini ,mamlaka yanabakia mikononi mwa mahakimu huru."

Alieshindwa katika hukumu iliotolewa ni waziri wa ndani Bw.Schäuble .Hayo ni maoni ya gazeti la FRANKFURTER RUNDSCHAU:

"Hukumu hiyo haitampendeza Bw.Schäuble.Waziri huyu mara nyingi akiikosoa hadharani Mahkama kuu ya shirikisho kwa hukumu iliotoa tangu kupinga kuwachunguza raia na hata kuziangusha ndege za abiria ikiwa zimetekwanyara na magaidi.

..........Hukumu ya Karlrsruhe ya kufuta kabisa sheria zake kunamuudhi zaidi waziri huyo kwavile, kunazifanya sheria zake anazotunga zisizipendeze kabisa kwa raia.Zamani waziri huyo wa nadni akitaka kuingilia mtandao wa internet ili kuuchunguza kinapita nini ndani yake....Sasa baada ya hukumu ya jana mipango ya Bw.Schäuble kutumia taarifa za wasafiri wa magari atabidi kuzirekebisha kabisa ili zichukue sura nyengine. "

Kwa jicho la STUTTGARTER ZEITUNG athari za hukumu ya Mahkama ya katiba zinakwenda mbali sana: Laandika:

"Hukumu ya Karlsruhe kimsingi,ni hukumu ya kujikinga na yale yanayoweza kutokea siku za mbele.Sheria ziliopo sasa tayari zinaruhusu mambo mengi kupita kiasi:zaruhusu kwa mfano, msako unaoendelea kwa msaada wa picha za nambari za magari yaliopo majiani.Kwa njia hii, picha zinaonesha kinachoendelea.Hata siku zijazo hii yawezekana kufanyika.Mahkama lakini inadai sheria kali na kutotumika kila mahala.

Hukumu iliotolewa jana kwahivyo, inapinga kuigeuza nchi hii kuwa dola linalowachunguza raia zake mfano kusajili nambari zao za magari.hukumu hiyo kwahivyo, athari zake zitapindukia mpaka wake."

Mwishoe gazeti la ALLGEMEINE ZEITUNG linalochapishwa mjini Mainz laandika:

"Pale watungaji sheria wakitaka siku zijazo kuepuka kuzimwa na Mahkama kuu kwa sheria wanazotunga ,wanapaswa kutia mno maanani haja ya kulinda taarufa zinazowahusu raia....."