Hujuma dhidi ya wahindi | Magazetini | DW | 23.08.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Magazetini

Hujuma dhidi ya wahindi

Shambulio la wafuasi wa mrengo wa kulia huko sachsen,mashariki mwa Ujerumani laendelea kugongwa vichwa vya habari na sio Ujerumani pekee bali hata India kwenyewe.

Kuandamwa kwa wahindi katika mkoa wa Sachsen,huko Mashariki mwa Ujerumani, kunaendelea kuchambuliwa na safu za wahariri wa magazeti ya Ujerumani.

Jicho hasa linatupwa juu ya maoni ya wanasiasa katika kile kinacho dhihirika dhahiri-shahiri ni hujuma ya chuki za kikabila.

Gazeti la FRANKFURTER ALLGEMEINE ZEITUNG juu ya mada hii linaandika:

Ali:”Kinachostusha mno sawa na kisa chenyewe kilichotokea huko Mügeln, ni muitiko uliogeuka sasa kuwa kama desturi.Wakati waziri mkuu Althaus anawakinga wajerumani mashariki kutotiwa wote chungu kimoja ,waziri mkuu Milbradt,anahofia dhara za kiuchumi za mkoa wake.

Siasa kali za bawa la mrengo wa kulia daima zadharauliwa na ndio maana katika miji midogo kama vile Mügeln,chuki hizo huongezeka na mwisho huripuka.”

Ni maoni ya Frankfurter Allgemeine Zeitung:

Ama gazeti la MANHEIMER MORGEN linahisi kila wakijongea zaidi kule mkasa huo ulikotokea, ndipo wanapozidi kuutoa maanani kuwa si kisa kikubwa.Gazeti laendelea:

Wanahofia hatari ya kupoteza heba ya mji huo namkoa mzima.Lakini, ni kwa kuzindukana wenye dhamana na kuwa tayari kulikabili tatizo lenyewe lilivyo, ndipo itakapowezekana kumtuliza shetani wa hisia za mchanganyiko wa chuki kwa raia wa kigeni,matumizi ya nguvu na siasa kali za mrengo wa kulia.Kuondoa kabisa chuki na siasa hizo haitawezekana ama Ujerumani mashariki au magharibi-

Ni maoni ya Mannheimer morgen.

Berliner Kurier linasema “ ili uweze kulitatua tatizo lolote, unabidi kwanza ulitambue tatizo lenyewe.Diwani-mkuu wa Mügelns,lakini, analifumbia macho tatizo lenyewe.” Gazeti linaonya:

“Kufanya hivyo, sio tu kuna dhara zake ,lakini pia ni kuonesha upumbavu wa hali ya juu.Wanasiasa wa mkoa wa Sachsen wanapotea njia katika kujieleza kwao wakikwepa kuzungumzia hasa siasa kali za mrengo wa kulia.Je, wanachunguza chanzo chake ? La hasha.

Kudai ‘wageni wote wafunge virago” aweza yeyote kuteleza na kusema hayo.” Lakini kwa njia hiyo, ndio unavumilia chuki kwa wageni.Kuna lakini wanasiasa waliokereka.Kuonesha kero wakati kwa wakati hakutoshi kupambana na mzizi wa fitina.

Kanzela Angela Merkel alihitaji siku 3 kufungua mdomo wake .Swali ni je, hakustahiki kuwa wa kwanza kulaanivisa hivyo ?

Ama gazeti la TAGESZEITUNG linalotoka Berlin laandika:

“Mawaziri wakuu waliohusika na kisa hiki wamenyamaa kimya.Wanasiasa wa vyama vyote katika shirikisho zima la Ujerumani, wamelaani matumizi ya nguvu kutoka mrengo wa kulia huko mashariki mwa Ujerumani.Wanadai hamasa zaidi za kidemokrasi na wanazungumzia kushindwa sehemu nyingi huko kujenga jamii za raia wenye nadharia za kidemokrasi.Ni Bibi Ursula von der Leyen, mwenye jukumu la kupambana na wafuasi wa mrengo wa kulia,hakutoa sauti yake.Na aseme nini ?