Houston, Texas , Marekani. Mtu mwingine ashambulia kwa risasi. | Habari za Ulimwengu | DW | 21.04.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

Houston, Texas , Marekani. Mtu mwingine ashambulia kwa risasi.

Marekani, ambayo imo bado katika kujiuliza kutokana na mauaji yaliyotokea katika chuo kikuu cha Virginia siku ya Jumatatu, imeshuhudia shambulio jingine la risasi, mara hii katika kituo cha utafiti wa anga cha NASA katika mji wa Houston katika jimbo la Texas.

Polisi wamesema kuwa mfanyakazi mkandarasi amemuua mtu mmoja aliyemteka nyara ndani ya jengo hilo la NASA na baadaye alijiua.

Polisi wamesema kuwa mtu wa pili aliyetekwa nyara, mwanamke , alikutwa yu hai akiwa amefungwa. Tukio hilo lilijitokeza wakati wa siku ya maombolezi siku ya Ijumaa kwa ajili ya watu 32 waliopigwa risasi na kufa siku ya Jumatatu katika chuo cha ufundi cha Virginia , mauaji yaliyofanywa na mwanafunzi raia wa Korea ya kusini, ambaye alikuwa na historia ya matatizo ya akili.

Familia ya Cho Seung-Hui imeomba msamaha kwa ajili ya maafa hayo, yaliyotokea katika viunga vya chuo hicho kikuu.

Jana Ijumaa kulikuwa pia na tahadhari ya kiusalama katika shule mjini Colorado na Califonia.

Matangazo

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com