Hezbollaha tayari kupigana vita na Israel | Habari za Ulimwengu | DW | 15.02.2008
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

Hezbollaha tayari kupigana vita na Israel

BEIRUT:

Kiongozi wa Hezbollah nchini Libanon,Hassan Nasrallah amesema,kundi lake lipo tayari kupigana vita dhidi ya Israel.Alitoa kitisho hicho kwa njia ya televisheni wakati wa mazishi ya mwasisi mmojawapo wa Hezbollah,Imad Mughniyah alieuawa siku ya Jumanne katika mji mkuu wa Syria,Damascus.Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran Manoucher Mottaki alihudhuria mazishi hayo.Mughniyah aliekuwa akisakwa na polisi ya kimataifa kwa mashtaka ya kuhusika na mashambulizi kadhaa ya kigaidi, aliuawa katika mripuko wa bomu ndani ya gari.

Hezbollah inaituhumu Israel kuwa imehusika na mauaji hayo,lakini Israel imepinga tuhuma hizo.Israel imeimarisha ulinzi katika balozi na taasisi zake kote duniani, ikihofia uwezekano wa kufanywa mashambulizi ya kulipiza kisasi.

Matangazo

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com