HARARE:Mabasi 49 ya abiria yakamatwa na polisi | Habari za Ulimwengu | DW | 12.07.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

HARARE:Mabasi 49 ya abiria yakamatwa na polisi

Mabasi 49 yamekamatwa na kuzuiliwa nchini Zimbabwe kufuatia agizo la serikali la kupunguza bei za bidhaa na huduma kwa nusu.Madereva wa mabasi hayo aidhja mkuu wa duka la bidhaa za nyumbani walikamatwa baada ya kuongeza nauli kinyume na agizo hilo la serikali.

Hatua hiyo imeathiri usafiri jana jioni mjini Harare huku wenye mabasi wengine wakiondoa magari yao barabarani ili kupinga nauli zilizotangazwa na serikali.Kulingana na wenye mabasi bei hizo haziwezi kugharamia hasara za usafiri.Mfumko wa bei umefikia asilimia alfu 5 kwa sasa.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com