HARARE:Askofu katika kashfa ya uzinzi | Habari za Ulimwengu | DW | 17.07.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

HARARE:Askofu katika kashfa ya uzinzi

Gazeti la serikali la Zimbabwe limechapisha picha inayomuonesha Askofu wa kanisa la Roman nchini humo Pius Ncube akiwa kitandani na mwanamke ambaye ni katibu mukhtasi katika ofisi yake.

Picha hiyo ilipigwa kwa kutumia kamera iliyofichwa chumbani humo, ikimuonesha askofu huyo akiwa hana nguo pamoja na mwanamke ambaye mumewe amefungua kesi dhidi ya Askofu huyo.

Askofu Ncube amekuwa akitoa shutuma kubwa dhidi ya utawala wa Rais Robert Mugabe.

Ubalozi wa Vatican mjini Harare umekataa kusema lolote juu ya kadhia hiyo ya kesi ya uzinzi kwa mtumishi wake.

Mapema mume wa mwanamke huyo ambaye ni katibu mukhtasi katika ofisi ya Askofu Ncube alifungua kesi ya madai katika mahakama ya Bulawayo akidai Askofu Ncube kuwa na uhusiano na mkewe kwa muda wa miaka miwili sasa.Anadai fidia ya dola laki moja na elfu 60.

Matangazo

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com