HANOI:Watu sio chini ya 60 wauwawa kwenye ajali ya kuporomoka daraja | Habari za Ulimwengu | DW | 26.09.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

HANOI:Watu sio chini ya 60 wauwawa kwenye ajali ya kuporomoka daraja

Kiasi cha watu 60 wameuwawa na wengine wengi wamejeruhiwa au kutoweka baada ya daraja walilokuwa wakilijenga huko kusini mwa Vietnam Kuanguka.

Hata hivyo idadi kamili ya watu waliokuwa wakifanya kazi ya ujenzi kwenye eneo hilo hii leo haijulikanai.Waokoaji wanaendelea kuchimba vifusi kwenye eneo hilo kuwatafuta manusura.Kwa mujibu wa taarifa za polisi nchini humo kulitokea kama mripuko na kisha daraja hilo likaporomoka.Ajali hiyo inasemekana kuwa kubwa zaidi kuwahi kutokea katika nchi hiyo.Ujenzi wa daraja hilo ni mradi unafadhiliwa na Japan na ulitarajiwa kukamilika mwaka ujao.

Matangazo

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com