Hali ya wasiwasi yawakabili Wakenya huku Onyancha akifikishwa mahakamani | Masuala ya Jamii | DW | 15.06.2010
 1. Inhalt
 2. Navigation
 3. Weitere Inhalte
 4. Metanavigation
 5. Suche
 6. Choose from 30 Languages

Masuala ya Jamii

Hali ya wasiwasi yawakabili Wakenya huku Onyancha akifikishwa mahakamani

Mshukiwa huyo anadai aliwaua watu 19 lakini alitaka kuua 100

Phillip Onyancha mwenye umri wa miaka 32, amefikishwa mahakamani hii leo kwa mauaji ya Anthony Njirua Muiruri. Polisi wanasema walimkamata jamaa huyo kwa kumteka nyara kijana huyo Muiruri, kwa kumfuatilia kupitia simu yake ya mkononi ambayo alikuwa akiitumia kuwashinikiza wazazi wake wamlipe fedha kabla kumuachilia. Polisi pia wanasema Onyancha amekiri alimua kijana huyo pamoja na watu wengine 18.

Akiwa mahakamani hii leo, Onyancha hakujibu mashitaka yanayomkabili kwa sababu hakuwa na wakili.

Habari za kutisha kuhusu jamaa huyo ambaye amejitokeza hadharani kukiri kwamba amekuwa akitekeleza mauaji ya kikatili, na kisha kunywa damu za watu hao, zinazidi kuzusha hofu kote nchini Kenya.

Sasa visa vya kupotea watu vimeanza kuhusishwa moja kwa moja na ukatili huo unaohofiwa umetekelezwa na wafuasi wa makundi yenye itikadi kali wanaotaka kumaliza kiu chao kwa kunywa damu ya wanadamu.

Mwandishi wetu Eric Ponda kutoka Mombasa ametuandalia taarifa ifuatayo.

Sauti na Vidio Kuhusu Mada

 • Tarehe 15.06.2010
 • Mwandishi Josephat Nyiro Charo
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo https://p.dw.com/p/NrXe
 • Tarehe 15.06.2010
 • Mwandishi Josephat Nyiro Charo
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo https://p.dw.com/p/NrXe
Matangazo

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com