Hali ya kisiasa ni tete Kyrgystan | Matukio ya Kisiasa | DW | 08.04.2010
 1. Inhalt
 2. Navigation
 3. Weitere Inhalte
 4. Metanavigation
 5. Suche
 6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Matukio ya Kisiasa

Hali ya kisiasa ni tete Kyrgystan

Serikali ya Kyrgyzstan imeangushwa na wapinzani baada ya mapambano makubwa baina ya wapinzani hao na maafisa wa usalama

Machafuko katika mji mkuu wa Kyrgystan, Bischkek

Machafuko katika mji mkuu wa Kyrgystan, Bischkek

Machafuko yaliyotokea nchini Kyrgyzstan ni matokoe ya hali ya kutoridhika miongoni mwa wananchi. Watu waliandamna kuupinga utawala wakifisadi wa rais Bakiyev uliokaa kufanya mazungumzo na wapinzani wa serikali yake.

Sababu ya kungushwa kwa utawala wake siyo rushwa tu. Ukosefu wa ajira katika nchi hiyo ya Asia ya kati umefikia kiwango cha juu sana na umasikini unazidi kuenea katika jamii. Kirgizstan inategemea misaada ya fedha kutoka kwa jumuiya ya kimataifa.Lakini fedha za msaada haziwaafikii wananchi na badala yake zilikuwa zinaingia katika mifuko ya rais Bakiyev na wapambe wake.Rais Kurmanbek Bakiyev aliingia madarakani miaka mitano iliyopita akiwa tumaini kubwa la watu wa Kirgizstan. Baada ya kuangushwa kwa utawala wa rais wahapo awali Akayev, Bakiyev aliingia madarakani na kuahidi kuleta mageuzi- Lakini ahadi hiyo ilikuwa kauli tupu kama anavyosema mkaazi mmoja wa mji wa Bishkek.

Baada ya rais wa zamani Akayev kukimbia tulimchagua Bakiyev.Tulikuwa na matumaini juu ya rais huyo mpya kuleta hali bora katika maisha yetu.Kumbe tulifanya kosa.Tulimchagua mtu fisadi.Bakiyev ana ndugu saba au wananane na wotewalikuwa wanajiingiza katika mambo y serikali na katika masuala ya kisiasa.Waliokuwa wanapitisha maamuzi ya serikali hawakuwa wakuu wa majimbo au mawaziri bali walikuwa ndugu zake Bakiyev.Hiyi ndiyo sababu kwamba sasa hatumtaki."

Naye Mwanaharakati wa haki za binadamu nchini Dianaraa amesema kuwa rais Bakiyev alijenga mfumo wa kikteta na alibana uhuru wa kutoa maoni na uhuru wa vyombo vya habari.

Katika siku za hivi karibuni , ilikuwa hatari kwa mtu kujaribu kuikosoa serikali.Na aliejaribu kufanya hivyo aliandamwa. Vitisho vilitolewa .Waandishi habari walivamiwa na walipigwa"

Serikali ya Bakiyev iitumia mabavu kuzima upinzani wa wananchi na viongozi wa upinzani walikamtwa na kwekwa ndani. Katika uchaguzi wa rais uliofanyika mwaka uliopita washindani wa Bakiyev hawakuwa hata na mwanya wa kushinda.Uchaguzzi huo ulifanyiwa mizengwe ya hali y a juu.

Ghadhabu za wananchi juu y rushwa, umasikini na udanganyifu wa kura tayari zilikuwa kubwa wakati serikali ya rais Bakiyev ilipoamua kupandisha bei ya nishati kuanzia mwezi januari. Maji yalifika utosini.Wapinzani walijianda na kuanza kumkabili Bakiyev kwa maandamano makubwa. yaliyowashangaza hata viongozi wa upinzani.

Kirgizstan ni nchi iliyopo mahala muhimu katika Asia ya kati ambapoMarekani ina kituo chaa kijeshi.

Kituo hicho ni muhimu kwa ajili ya kukidhi mahitaji yanayohitijika katika vita vya nchini Afghanistan.

Urusi pia ina kituo cha kijeshi nchini Kirgizstan.Marekani inaizingatia Kirgizstan kuwa nchi muhimu katika vita vya kupambana na ugaidi katika Asia ya kati.

Mwandishi/Christina Lage/ZA

Tafsiri/Mtullya Abdu.

Mpitiaji:Sekione Kitojo

 • Tarehe 08.04.2010
 • Mwandishi Josephat Nyiro Charo
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo https://p.dw.com/p/MqYf
 • Tarehe 08.04.2010
 • Mwandishi Josephat Nyiro Charo
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo https://p.dw.com/p/MqYf
Matangazo

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com