Hali ya kisiasa nchini Kenya
22 Februari 2008Matangazo
Mazungumzo ya kutafuta amani yanayoendelea kwa yapata majuma mawili yameingia hatua nyeti chini ya uongozi wa katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa wa zamani Koffi Annan. Wakati huo huo kiongozi wa chama cha Orange Democratic Movement ODM Bw.Raila Odinga anaripotiwa kuondoka nchini kwa ndege binafsi na kutarajiwa kurudi hapo kesho. Kwa mujibu wa mfanyakazi mmoja katika uwanja wa ndege, Bw.Odinga ameelekea nchini Nigeria.
Ili kupata thibitisho kuhusu taarifa hizo Thelma Mwadzaya alizungumza na William Ruto mmoja wa viongozi wa chama cha ODM aliye pia mbunge wa Eldoret Kaskazini.