Hali ya kisiasa katika kisiwa cha Nzouani baada ya kufanya uchaguzi wa rais kwa lazima | Matukio ya Kisiasa | DW | 14.06.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Matukio ya Kisiasa

Hali ya kisiasa katika kisiwa cha Nzouani baada ya kufanya uchaguzi wa rais kwa lazima

Uongozi visiwani Komoro vinatangaza kuwa huenda ukachukulia kisiwa cha Nzouani hatua za kijeshi kwa kufanya uchaguzi wa rais kwa lazima ulioahirishwa kwa juma moja na serikali kuu.

Uchaguzi huo ulipangwa kufanyika Jumapili iliyopita lakini kuahirishwa hadi tarehe 17 mwezi huu kwa sababu za kiusalama. Tume ya uchaguzi ya Nzouani ilikiuka agizo hilo na kufanya uchaguzi na kumtangaza raia wa zamani wa kisiwa hicho Mohamed Bakary mshindi. Mohamed Bakary aliingia madarakani baada ya kupindua serikali mwezi Agosti mwaka 2001 na kuongoza kwa muhula wa miaka mitano mwaka uliofuatia. Hasa hatua za kijeshi zina maana gani dhidi ya Nzouani? Thelma Mwadzaya alimuuliza Ibrahim Abdalla mshauri wa rais wa serikali kuu ya Komoro Abdalla Sambi.
Matangazo

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com