Hali Baghdad yaanza kurejea ya kawaida | Matukio ya Kisiasa | DW | 17.12.2007
 1. Inhalt
 2. Navigation
 3. Weitere Inhalte
 4. Metanavigation
 5. Suche
 6. Choose from 30 Languages

Matukio ya Kisiasa

Hali Baghdad yaanza kurejea ya kawaida

Miaka minne baada ya vita nchini Iraq na kukaliwa na mejejshi yaliyoongozwa na Marekani, kuna ishara kuwa sasa maisha yanaanza taratibu kurejea ya kawaida.

default

Wananchi wa Baghdad wakifanyiwa upekuzi na vikosi vya Marekani

Hii ni baada ya kuwasili mjini Baghdad kwa kikosi cha ziada cha wanajeshi elfu 37 wa Marekani mwezi June mwaka huu.

Hata hivyo mwaka huu unakaokaribia kumaliza, nchi yote kwa ujumla imeendelea kubakia katika dimbwi la vurugu, ghasia na woga, vyote hivyo vikiendelea kukwamisha kuimarika kwa mfumo wa kisiasa.

Kazem Hassan mkaazi wa jijini Baghdad anasema kuwa kwa mara ya kwanza toka mtoto wake mwenye umri wa miaka minne alipozaliwa sasa anaweza kufurahia maisha kama mtoto ya kucheza.

Anasema mchezo kama wa kubembea alikuwa akiuona kwenye runinga tu, lakini sasa wanaweza kwenda naye nje kwenye bustani na kucheza kwenye mabembeya.

Maneno hayo ya Kazem yanathibisha kauli za wakaazi wengi wa Baghdad kuwa maisha sasa yameanza kurejea katika hali ya kawaida mjini humo toka kuwasili kwa kikosi cha ziada cha wanajeshi wa Marekani.Hivi sasa kuna kiasi cha wanajeshi laki moja na elfu 62 wa Marekani mjini humo.

Mashambulizi ya mabomu iwe ya kujitoa mhanga au ya kwenye magari yamepungua kwa takriban nusu nzima toka kuwasili kwa askari hao wa ziada.

Kwa mara ya kwanza katika kipindi cha miaka miwili hivi sasa wananchi wanaweza kwenda katika bustani, kufanya manunuzi au kwenda kazini katika maeneo ya washia na wasunni.Pia wakaazi hao wamekuwa wakifanya matembezi ya usiku kinyume na ilivyokuwa hapo kabla.

Kurejea nyumbani kwa watu laki mbili jijini humo ni ishara nyingine ya kutengemaa kwa hali ya usalama.

Hata hivyo mpango wa muda mrefu wa kuirejesha nchi hiyo katika amani, umendelea kutokuwa na uhakika, kwani mafanikio ya kisiasa hayaendani na mafanikio yaliyofikiwa na jeshi la Marekani pamoja na la Iraq mwaka huu.

Profesa Hamid Fadhil ambaye ni mhadhari wa sayansi ya siasa katika chuo kikuu cha Baghdad anaonya ya kwamba kwa kufanikiwa katika kudhibiti usalama jijini Baghdad na katika miji mingine, ni lazima sasa wafikirie kuimarisha mfumo wa siasa.

Profesa huyo anasema mafanikio hayo kidogo katika kudhibiti usalama , yatawapotosha wairaq na kuitumbukiza nchi hiyo katika mgawanyiko wa majimbo ya kiuhasama na kushindwa kushughulikia masuala muhimu na ya kimsingi.

Miongoni mwa masuala hayo ni kufikiwa kwa muafaka juu ya utungaji wa vifungu 20 vya sheria kama vile sheria inayodhibiti mafuta, na gesi, pamoja na kurejeshwa kwenye ajira za serikali maelfu ya wanachama wa chama Baath cha Saddam Hussein.

Mpaka sasa serikali ya kitaifa nchini humo inaundwa na muungano wa vyama viwili vya washia na wakurdi.Hata hivyo kujitoa kwa mawaziri wengi ambao ni wa kutoka upande wa washia, kuimeifanya serikali ikaribie kuanguka.

Hali hii inazidishwa na harakati za majimbo nchini humo ambayo yanataka kujitenga na kujitawala, ambayo yanaioana serikali kuu ya Baghdad isiyostahiki kutawala.

Katika eneo la Kaskazini ambalo ni la wakurdi serikali ya eneo hilo, imebadilisha sera na siasa zake kuelekea katika kujitawala kwani imepitisha sheria zake katika masuala ya mafuta na gesi na imefunga mikataba ya kibiashara.

Huko Kusini waasi wa kishia wanapigana kutaka kudhibiti jimbo lenye utajiri mkubwa wa mafuta la Basra.Basra ni mji wa pili kwa ukubwa nchini humo na ndiyo jimbo pekee lenye bandari.

Mkuu wa Polisi wa jimbo hilo Meja Jenerali Jalil Khalaf amesema kuwa idadi kubwa ya bandari za jimbo hilo ziko chini ya udhibiti wa wapiganaji hao.

Vikosi vya jeshi la Uingereza vilivyokuwa katika mji huo, wiki hii vimekabidhi mamlaka ya ulinzi kwa jeshi la Iraq, hali inayotoa wasi wasi wa kuwepo mwanya kwa waasi hao kuimarisha zaidi harakati zao.

Wasunni ambao wanaungwa mkono na Marekani, wameanzisha kitu kinachoitwa Baraza la Uamsho kupambana na wapiganaji wa al-Qaida pamoja na wanamgambo mahafidhina kwenye majimbo ya nchi hiyo.

Harakati zao katika miji ya Diyala, al-Anbar na Baghdad zimezaa matunda na kwa kiwango fulani kwani usalama umeimarika.

Lakini taarifa za kijasusi nchini humo zinaonya kuwa msaada wa majeshi ya Marekani unaweza kuimarisha serikali za majimbo na kuidhoofisha serikali kuu ya Baghdad. Mchanganyiko huo wa ishara za mafanikio na changamoto zilizo mbele, vinaonekana na baadhi ya wadadisi wa mambo kama ni tumaini kwa mwaka ujayo, ikitiliwa maanani ya kwamba serikali imetangaza bejeti kubwa katika historia ya

 • Tarehe 17.12.2007
 • Mwandishi Aboubakary Liongo
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo https://p.dw.com/p/CcoJ
 • Tarehe 17.12.2007
 • Mwandishi Aboubakary Liongo
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo https://p.dw.com/p/CcoJ

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com