Goma, Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo. Nkunda atangaza vita na majeshi ya serikali. | Habari za Ulimwengu | DW | 09.10.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

Goma, Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo. Nkunda atangaza vita na majeshi ya serikali.

Kiongozi wa waasi katika eneo la mashariki mwa jamhuri ya kidemokrasi ya Kongo DRC ametangaza kuwa majeshi yake yatafanya mashambulizi dhidi ya majeshi ya serikali. Jenerali huyo muasi Laurent Nkunda amesema kuwa wapiganaji wake waasi wametupilia mbali makubaliano ya kusitisha mapigano yaliyodumu kwa muda wa mwezi mmoja nchini DRC. Mapigano mapya yalizuka siku ya Alhamis na yanaendelea hadi leo.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com