Fukushima, hatari ya kuyeyuka nyuklia ingalipo nchini Japan | Matukio ya Kisiasa | DW | 27.03.2011
 1. Inhalt
 2. Navigation
 3. Weitere Inhalte
 4. Metanavigation
 5. Suche
 6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Matukio ya Kisiasa

Fukushima, hatari ya kuyeyuka nyuklia ingalipo nchini Japan

Hatari ya kuyeyuka nyuklia kwenye kinu nambari 2 bado ni kubwa nchini Japan.

Wafanyakazi wakijaribu kukirekebisha kinu cha nyuklia,nchini Japan

Wafanyakazi wakijaribu kukirekebisha kinu cha nyuklia,nchini Japan

Kiwango cha mionzi kimeongezeka kwenye kinu cha nyuklia nambari 2 cha Fukushima nchini Japan.

Kwa mujibu wa wahusika kiwango hicho kimevuka kile cha kawaida mara milioni kumi.Wafanyakazi waliokuwa wanajaribu kukirebisha kinu hicho kilichoharibika sana baada ya kukumbwa na maafa wamelazimika kuondolewa na kupelekwa kwenye sehemu salama.

Kampuni inayokiendesha kinu hicho, ya Tokyo Electric, TEPCO imearifu kuwa maji yalioingia mionzi yamo chini ya injini iliyopo katika jengo lililounganishwa na kinu hicho nambari 2.Kinu hicho kilichopo Fukushima kiliharibiwa vibaya kutokana na mitetemeko ya ardhi na Tsunami wiki mbili zilizopita.Kampuni ya TEPCO imejaribu kuyaondoa maji yaliyoingia mionzi ya nyuklia kwenye vinu vinne vya Fukushima.

Wakati huo huo mashirika ya habari yamearifu kuwa hatari ya kutokea maafa makubwa ya kuyeyuka kwa nyuklia bado ingalipo.

 • Tarehe 27.03.2011
 • Mwandishi Abdu Said Mtullya
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo https://p.dw.com/p/10iAL
 • Tarehe 27.03.2011
 • Mwandishi Abdu Said Mtullya
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo https://p.dw.com/p/10iAL