FRANKFURT:Mauzo ya BMW yaongezeka | Habari za Ulimwengu | DW | 06.07.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Habari za Ulimwengu

FRANKFURT:Mauzo ya BMW yaongezeka

Kampuni ya kutengeza magari ya BMW ya hapa Ujerumani inatangaza kuwa pato la magari limeongezeka kwa asilimia 4.5 katika kipindi cha miezi sita ya mwanzo wa mwaka huu.Kampuni hiyo iliyo na makao yake mjini Munich imeuza magari laki saba thelathini aina ya BMW,Mini na Rolls Royce kuanzia mwezi wa Januari hadi mwezi huu wa Juni ikilinganishwa na magari laki sita tisaini na nane mwaka jana.

Mwezi jana pekee kampuni hiyo imeuza magari laki moja unusu kote ulimwenguni ikiwa ni ongezeko la asilimia 15.1 ikilinganishwa na mwezi Juni mwaka jana.Idadi ya magari yaliyouzwa nchini Uchina,Urusi na Ulaya magharibi imeongeza mauzo kwa jumla ya mwezi Juni.

Matangazo

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com