Fiji yatangaza hali ya hatari | Habari za Ulimwengu | DW | 06.12.2006
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

Fiji yatangaza hali ya hatari

Kiongozi wa jeshi kisiwani Fiji Kamanda Frank Bainimarama anasema kwamba majeshi yake yatadhibiti nchi hiyo endapo vurugu zozote zitatokea baada ya mamlaka kubadilika.Hatua hiyo inatokea baada ya waziri mkuu aliyengolewa madarakani Laisenia Qarase kutoa wito wa kufanyika maandamano ya amani.

Kiongozi huyo wa zamani alisindikizwa nje ya mji mkuu na polisi waliojihami kwa sialaha.Kiongozi huyo wa jeshi ametangaza hali ya hatari siku moja baada ya kuchukua hatamu za uongozi.Bwana Bainimarama amevunja bunge vilevile kuteua waziri mkuu wa muda katika kipindi hicho.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com