DUBAI:Sauti inayodaiwa kuwa ya Osama yawashauri wanamgambo Iraq kushirikiana | Habari za Ulimwengu | DW | 23.10.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

DUBAI:Sauti inayodaiwa kuwa ya Osama yawashauri wanamgambo Iraq kushirikiana

Kituo cha Televisheni cha kiarabu cha Al Jazeera kimerusha Ukanda wa sauti unaodaiwa kuwa na sauti ya kiongozi wa mtandao wa Al Qaeda Osama Bin Laden.Katika ukanda huo Osama ameyatolea mwito makundi ya wanamgambo nchini Iraq kuondoa tafauti zao na kuungana katika kulikomboa taifa hilo.

Sauti hiyo pia imeonya dhidi ya majaribio ya maadui ya kutaka kutia dosari kati ya makundi hayo kwa kupachika mawakala wao ndani ya makundi hayo.

Hata hivyo haijakuwa wazi ni lini ukanda huo ulirekodiwa lakini wamchambuzi wa mambo wanasema sauti iliyosikika kwenye ukanda huo huenda ikawa kweli ni ya Osama Bin Laden ingawa hilo halijathibitishwa.

Matangazo

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com