1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

DRC: Vituo 38 vya Radio na Televisheni vyapigwa maarufu

22 Oktoba 2007

Vituo 38 vya RAdio na Televisheni vya kibinafsi vikiwemo vile vya Jean Pierre Bembe vimepigwa maarufuku kutangaza katika Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo.

https://p.dw.com/p/C7gi

Hatua hiyo imechukuliwa na waziri wa habari wa nchi hiyo ambaye amewalaumu viongozi wa vituo hivyo kwa kutodumisha nidhamu na vituo vingine vimekuwa vikiendeleza kazi zake bila leseni ya utangazaji.

Shirika la kutetea haki za waandishi wa habari nchini humo limepinga vikali hatua hiyo.

Mwandishi wetu Saleh Mwanamlongo anaripoti zaidi kutoka Kinshasa.