Dominique Strauss-Kahn aachiliwa huru kwa mashtaka ya ngono | Matukio ya Kisiasa | DW | 24.08.2011
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Matukio ya Kisiasa

Dominique Strauss-Kahn aachiliwa huru kwa mashtaka ya ngono

Hakimu mjini New York, Marekani, aliyatupilia mbali mashtaka ya ngono yaliomkabili mkuu wa zamani wa IMF, Dominique Strauss-Khan, hivyo kulimalizika lile sakata la udhalilishaji lilioharibu sifa ya mtu huyo.

default

Dominique Strauss-Kahn na wakili wake wakiwa mahakamani

Jaji Michael Obus alilikubali ombi la mwendeshaji mashtaka la kuachana na kesi hiyo ambayo wameiona haiwezekani kushinda kutokana na mshtaki- mtumishi wa hoteli, Nafissatou Diallo, aliyemtuhumu Strauss-Kahn kufanya nae ngono kwa nguvu- kuwa alisema uwongo mara kadhaa, hivyo haaminiki. Strauss-Kahn, akitoka mahakamani na mkewe, Anne Sinclair, ambaye katika wakati wote tangu kashfa hiyo kujulikana, amemtea mumewe na kusema hana hatia, alisema amepumua na kumshukuru mkewe, watoto wake na kila mtu aliyemuunga mkono. Punde hivi Othman Miraji alizungumza na mwandishi wa habari wa mjini Paris, Mohammed Saleh, juu ya vipi wafaransa walivopokea habari za kuachiliwa huru Dominique Strauss-Kahn...

Mwandishi: Othman Miraji

Mhariri: Mohamed Abdulrahman

Matangazo

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com