Copenhagen. Chama cha waziri mkuu chapata ushindi. | Habari za Ulimwengu | DW | 14.11.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

Copenhagen. Chama cha waziri mkuu chapata ushindi.

Waziri mkuu wa Denmark Anders Fogh Rasmussen ametangaza ushindi katika uchaguzi uliofanyika jana Jumanne baada ya matokeo kukaribia kukamilika ambapo inaonyesha kuwa serikali yake ya mrengo wa kati kulia imepata ushindi mwembamba na kuushinda upande wa upinzani wa mrengo wa shoto.

Wakati kura karibu zote zimekwisha hesabiwa , muungano wa kiliberali na kihafidhina wa Rasmussen pamoja na chama cha mrengo wa kulia cha Danish Peoples Party wana viti 90 katika bunge. Wakati ushindi kamili wa kundi hilo ukiwa katika shaka shaka hapo mapema wakati wa kuhesabu kura, lilihakikisha ushindi baada ya chama kinachosaidia muungano huo kupata kiti kimoja kati ya viwili katika eneo la Denmark la visiwa vya Faroe. Waziri mkuu ameitisha uchaguzi zaidi ya mwaka mmoja kabla akitumaini kuwa uchumi imara utasaidia kumpa ushindi na kutumikia kipindi cha awamu wa tatu kabla ya majadiliano magumu ya mishahara ya sekta ya umma kuanza mwaka ujao.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com