1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

China: China, Ujerumani kuendelea na biashara wazi na huria

Sudi Mnette
18 Februari 2024

Waziri wa Mambo ya Nje wa China Wang Yi amesema China na Ujerumani zinapaswa "kuepuka kuingiliwa kati" na kuendelea na biashara yenye uwazi na uhuru.

https://p.dw.com/p/4cXfi
Ujerumani | Mkutano wa Usalama wa Munich | Wang Yi, Waziri wa Mambo ya Nje wa China
Mkutano wa Usalama wa Munich Wang Yi, Waziri wa Mambo ya Nje wa China - Februari 17, 2024 MunichPicha: Frank Hofmann/DW

Waziri wa Mambo ya Nje wa China Wang Yi amesema China na Ujerumani zinapaswa "kuepuka kuingiliwa kati" na kuendelea na biashara yenye uwazi na uhuru baina yao.Kwa mujibu wa wizara ya mambo ya nje ya China kauli hiyo ni matokeo ya mazungumzo na Kansela wa Ujerumamani Olaf Scholz katika Mkutano wa Kimataifa wa Usalama wa Munich ambao unafikia kilele chake leo hii. Mkutano wa Munich ulianza Ijumaa ya Februari 16, unafikia kilele chake leo.