Chelsea ya umana na Manchester united | Michezo | DW | 09.01.2009
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Michezo

Chelsea ya umana na Manchester united

Marudio ya finali ya champions League katika Premier League:

Michael BALLACK baada ya kulazwa na Manu,

Michael BALLACK baada ya kulazwa na Manu,

Katika changamoto za Premier League,kesho ni marudio ya finali ya mwaka uliopita ya Kombe la klabu bingwa barani Ulaya-champions League kati ya mabingwa Manchester United na Chelsea-

Kinyanganyiro cha kombe la Cecafa-Challenge Cup kinaendelea nchini Uganda-nani mwishoe ataibuka bingwa ?

Tuanze na Ligi mashuhuri barani Ulaya kabla hatukujiunga na George Njongopa huko Dar-es-salłaam, akitufungulia pazia la changamoto za Kombe la Challenge-Kombe la CECAFA huko Kampala ,Uganda.

Jane Nyingi anawachukua kwanza katika Premier League-Ligi ya Uingereza na mpambano wa kesho wa kukata na shoka kati ya mabingwa wa dunia,Ulaya na Uingereza, Manchester United na Chelsea-marudio ya finali ya mwaka jana ya Kombe la klabu bingwa barani Ulaya:

Kocha wa Chelsea, mbrazil Luiz Felipe Scolari, ameungama hivi punde kwamba Chelsea kesho lazima ithibitishe imekomaa katika dimba kwa kuondoka na ushindi mbele ya mabingwa, Manchester.Kwani, Chelsea bado haikutamba mbele ya mahasimu wake 4 wakubwa katika Premier League-tangu Scolari kuwa kocha. Chelsea iko pointi 4 usoni kuliko Manchester United huku ikifuatia Liverpool inayoongoza kwa pointi 3. Endapo Manu ikishinda kesho basi itapunguza mwanya hadi pointi 1 kati yake na Chelsea na hiyo ndio shabaha ya kocha wa Manu Sir Alex Ferguson.

Inatazamiwa mashabiki kote duniani watakodoa macho au kutega sikio katika mpambano huu na mbrazil Scolari atataka kuona kikosi chake kinatamba mbele ya mabingwa wa dunia -Manchester United. Leo viongozi wa Ligi Liverpool wamepanga miadi na Stoke City wakati Arsenal wanacheza na Bolton Wanderers.

Arsenal jana ilionesha iko karibu kukamilisha mkataba na stadi wa dimba wa Urusi alietamba mwaka jana katika kombe la Ulaya la mataifa, Andrei Arshavin.Kocha wa Arsenal, Arsene Wenger, amekuwa akimsaka sana stadi huyo wa Zenit St.Petersberg. Arsenal inatarajiwa kulipa kitita cha pauni milioni 20 kumkomboa Arshavin.

Katika Serie A, Ligi ya Itali,kikosi cha washambulizi 3 wa Brazil-akina Kaka,Ronaldinho na Pato, kimejiwinda kuzima vishindo vya Roma nyumbani mjini Rome kesho na kuondoka na ushindi kwa trimu yao ya AC Milan.Milan iko nafasi ya 3 katika ngazi ya Ligi ya Itali wakati Roma iko pointi 23 kutoka viongozi wa Ligi Inter Milan.Juventus wako nafasi ya pili.

Macho ya mashabiki yataukodolea macho mpambano huu kujua iwapo stadi na nahodha wa zamani wa Uingereza, David Bekham, atachezeshwa na AC Milan alao kwa muda mfupi.Beki wa zamani wa timu ya Taifa ya Marekani, Alexi Lalas, amesema hangeshangaa kuona David Bekham, hatarejea Marekani kutoka Itali kuichezea klabu yake ya Los Angeles Galaxy. Bekham ameazimwa kwa Milan kwa miezi 2 na akitarajiwa kurejea Los Angeles Machi ijayo.

Ama katika La Liga, Ligi ya Spain, FC Barcelona inarudi uwanjani kesho kuendelea kutamba kama ilivyotamba 2008.Baada ya kuwachapa mahasimu wao wakubwa Real Madrid mabao 3-1 kabla kuingia mwaka mpya, Barcelona ina miadi kesho na Osasuna inayoburura mkia wa Ligi.

Barcelona wamefungua mwanya wa kiasi cha pointi 12 kileleni na takriban wameshatia mfukoni taji la msimu huu.

Leo Deportivo La Coruna wana miadi na Sevilla wakati Valencia wanacheza na Villarreal.

Kinyanganyiro cha kumsaka bingwa wa Kombe la Cecafa-kanda ya Afrika Mashariki na kati kinaendelea mjini Kampala,Uganda.Baada ya changamoto za jana ijumaa zilizoingiza timu 2 za Tanzania bara na visiwani,kesho Tanzania-bara ina miadi na harambee Stars (Kenya -mpambano wa nusu-finali.Mabingwa Sudan wametolewa na mapema kama pia Zambia-timu zilizotamba miaka ya nyuma.