Chama cha waziri mkuu wa zamani chashinda. | Habari za Ulimwengu | DW | 24.12.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Habari za Ulimwengu

Chama cha waziri mkuu wa zamani chashinda.

Bangkok. Chama kinachohusiana na waziri mkuu aliyeondolewa madarakani Thaksin Shinawatra kimedai kupata ushindi katika uchaguzi wa jana Jumapili wa bunge. Chama cha Peoples Power, PPP, hata hivyo , kimeshindwa kupata wingi mkubwa katika uchaguzi wa kwanza tangu kiongozi wake Thaksin alipopinduliwa miezi 15 iliyopita. Samak Sundaravej wa chama cha PPP amesema kuwa atajaribu kuunda serikali mpya na kumtaka Thaksin kurejea kutoka uhamishoni anakoishi hivi sasa. Haijafahamika iwapo waziri huyo mkuu wa zamani anaweza kutoa mchango wa aina yoyote kisiasa kwasababu amepigwa marufuku kwa muda wa miaka mitano kutoshiriki masuala ya kisiasa. Matokeo hayo ni pigo kwa jeshi la nchi hiyo ambalo lilijaribu kuzuwia ushawishi wa Thaksin katika nchi hiyo.

Matangazo

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com