Chama cha AfD chaongoza katika utafiti wa kitaifa wa YouGov
17 Septemba 2025
Matangazo
AfD ilipata asilimia mbili zaidi ya pointi ikilinganishwa na utafiti wa mwezi Agosti, na kuongeza umaarufu wake hadi 27%, huku muungano huo wa CDU/CSU ukishuka kwa pointi moja hadi 26%.
Kulingana na utafiti huo wa youGov, ikiwa uchaguzi mkuu ungefanyika Jumapili hii, chama cha mrengo wa kushoto cha Social Democrats (SPD), mshirika mdogo katika serikali, kingepata asilimia 15% ya kura, ambayo ni ongezeko la asilimia 1 na kile cha kijani kusalia katika asilimia 11.
Katika tafiti za hivi majuzi za taasisi nyingine za upigaji kura, AfD ilikuwa kwenye kiwango sawa ama nyuma tu kidogo ya muungano huo wa kihafidhina.