Chadema: Hatukuwaidhinisha wabunge walioapishwa | Matukio ya Afrika | DW | 25.11.2020
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Matukio ya Afrika

Chadema: Hatukuwaidhinisha wabunge walioapishwa

Chama kikuu cha upinzani nchini Tanzania Chadema, kimekanusha kuwaidhinisha wananchama wake kumi na tisa walioapishwa jana kama wabunge wa viti maalum na spika wa bunge.

Chama cha Chadema sasa kimewataka wabunge hao kufika mbele ya kamati kuu ya chama haraka iwezekanavyo kwa ajili ya kujieleza kabla ya hatua zaidi kuchukuliwa dhidi yao.

Akizungumza na waandishi wa habari muda mfupi uliopita katibu mkuuu wa chama hicho John Mnyika, amesema kilichofanyika jana ni biashara haramu iliohusisha mamlaka yenye lengo la kufifisha mjadala kuhusu kile alichokiita uchafuzi kwa jina la uchaguzi uliofanyika Oktoba 28.

Mnyika amesema kamati kuu ya chama ambayo inadhamana ya kupokea maombi, kupitia na kufanya uteuzi wa wabunge wa viti maalumu haikufanya mchakato huo, kutokana na chama hicho kutangaza hadharani kutoyambua matokeo ya uchaguzi uliomrejesha madarakani rais John magufuli na kupita kwa idadi kubwa ya wabunge kutoka chama cha mapinduzi CCM.

Tazama vidio 03:00

Chadema chawataka wake waloapishwa kama wabunge kujieleza

Aidha katibu huyo mkuu ambae pia amehudumu kama mbunge kwa miaka kumi, amewataja wabunge hao walioapishwa kama waasi na wasaliti wa democrasia aliodai imehafuliwa kwa ukiukwaji wa katiba.

Soma pia: Ukandamizaji ulihujumu uchaguzi Tanzania

Mapema mwezi Novemba mkurugenzi wa uchaguzi Charles Mahera alinukuliwa na vypombo vya habari, akisema chama hicho kikuu cha upinzani kimewasilisha majina ya wabunge wa viti maalum. Hata hivyo mnyika ameonesha mbele ya wanahabari barua za mawasiliano kati yake na NEC akikanusha uwasilishaji huo wa majina na barua ya mkurugenzi ambamo alikiri chama kutowasilisha majina.

Kwa mujibu wa ibara ya 78 ya katiba ya nchi, kipengele cha 3, majina ya watu yaliopendekezwa kwa mujibu wa ibara ndogo ya kwanza na tume ya taifa ya uchaguzi yatatangazwa baada ya NEC kuridhika kwamba masharit ya katiba na sheria yamezingatiwa.

Chama cha Chadema chasema, hakuwapa wanachama wake walioapishwa idhini ya kuwakilisha chama katika viti maalum bungeni.

Chama cha Chadema chasema, hakuwapa wanachama wake walioapishwa idhini ya kuwakilisha chama katika viti maalum bungeni.

Mnyika amesema hayo yote hayakuzingatiwa na kuhoji utaratibu uliofatwa kabla ya kuwaapisha wabunge hao, ambao walisema wanabaraka zote za chama na mwenyekiti wa chama hicho Freema Mbowe.

Mvutano huu umetajwa na raia kuwa huenda ukawa mwanzo wa kukisambaratisha chama hicho kikuu cha upinzani ambacho tayari kilipata pigo kubwa kwa kupata mbunge mmoja tu wa kuchaguliwa jimboni katika uchaguzi uliopita jambo ambalo wanasisitiza lazima kuwepo na mazungumzo baina ya wahusika.

Kamati kuu ya chama itaketi kwa dharura siku ya ijumaa ambapo pamoja na kuwatumia barua rasmi katibu mkuu wa chama hicho ametoa mwito wa wazi kwa wananchama wote walioapishwa kuhudhuria bila kukosa.

Sikiliza sauti 09:45

Kinagaubaga na mbunge pekee wa CHADEMA nchini Tanzania