Chad hali ya hatari | Matukio ya Kisiasa | DW | 15.02.2008
 1. Inhalt
 2. Navigation
 3. Weitere Inhalte
 4. Metanavigation
 5. Suche
 6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Matukio ya Kisiasa

Chad hali ya hatari

Amri ya kutotoka nje imetangazwa nchini Chad.

Rais Idris Deby wa Chad-kulia.

Rais Idris Deby wa Chad-kulia.

Amri ya hali ya hatari imetangazwa nchini Chad na kiongozi wa nchi hiyo kufuatia waasi kuushambulia mji mkuu wa nchi hiyo N'djamena mapema mwezi huu.


Hali ya hatari imetangazwa na rais Idris Derby wa nchi hiyo.Amri hiyo ya siku 15,inaanza kutumika leo na inahusu nchi nzima.


Akitangaza amri hiyo-rais Derby amesema kuwa amelezemika kuchukua hatua hiyo ili kuimarisha ulinzi na usalama kufuatia mashambulizi ya waasi,wanaompinga, katika mji huo mwezi uliopita.


Waasi wanaokadiriwa kufikia elf 3000 waliuzingira mji huo na kuikaribia ikulu kwa lengo la kumuondoa Derby kutoka madarakani.Lakini majeshi matiifu kwa serikali yake yaliwarejesha nyuma waasi hao.

Katika mapigano hayo inasemekana takriban 160waliuawa.

Katika taarifa yake kwa taifa kupita televisheni na Redio-rais Derby amesema kuwa ingawa waasi walifurushwa hadi katikati ya jangwa nchini humo,hatua muhimu zinahitajika ili kurejesha usalama wa taifa baada ya jaribio la mapinduzi.

Amri ya kutotoka nje usiku kuanzia saa sita za usiku hadi alfajiri ambayo imekuwepo katika mji mkuu tangu jaribio la waasi la mwezi jana ,sasa imeenezwa nchi nzima.

a

Amri ya rais hiyo inatoa ruhusa kwa nyumba kupekuli na pia kudhibiti vyombo vya habari.

Katiba ya nchi hiyo inamruhusu rais kuchukua hatua kama hiyo.Ibara ya katiba ya taifa inampa uwezo rais kuchukua hatua madhubuti kwa lengo la kulinda taifa.

Amri kama iliochukuliwa na rais ya kutotembea usiku inatakiwa kukubaliwa na bunge la taifa endapo mda wa siku 15 utamalizika.


Rais Derby amesema kuwa ataunda tume ya kirais kufuatilia utekelezwaji wa hatua hiyo,mkiwemo hatua dhidi ya usafiri wa watu.


Rais Derby ni rubani wa ndege za helikopta ambae alipata mafunzo kutoka Ufaransa.Ameiongoza nchi hiyo kwa miaka 18 sasa.Mara ya mwisho kutangaza amri ya kutotembea usiku ulikuwa mwaka wa 2006 baada ya mji mkuu wa N'djamena kushambuliwa na waasi wa ushirika wenye makao yao makuu katika mkoa wa Sudan wa Darfur.


Wiki moja iliopita,serikali ilitangaza amri ya kutotembea usiku katika mji mkuu na sehemu za mashariki na kati za nchi hiyo.Waasi waliposhindwa kuuteka kabisa mji wa N'djamena-walirejea nyuma katika maeneo ya mashariki ya nchi hiyo, huku wakiilaumu Ufaransa kwa kuuunga mkono kijeshi rais Derby ili kuweza kuwafurusha.


Serikali ya Ufaransa ili kiri kwa kusafirisha silaha kutoka Libya hadi Chad,lakini kukanusha madai kuwa wanajeshi wake walihusika katika mapigano.


Mapema wiki hii, Ufaransa ilitaka kujua majaliwa ya viongozi wa upande wa upinzani wa Chad waliokamatwa na wanajeshi wakati wa mapigano ya mjini N'djamena.Waziri wa mambo ya ndani-Mahamat Ahmat Bachir alisema kuwa walichukuliwa kutoka katika maeneo yaliyo kuwa yamechukuliwa na waasi na kuongeza kuwa serikali imeunda tume ya kuwafanyia uchunguzi.

Lakini hiyo jana waziri wa mambo ya ndani alisema kuwa mmoja wa viongozi watatu wa upinzani amepatikana akiwa mzima baada ya kupotea tangu mapigano ya Febuari 3.Kiongozi huyo aliepatikana ni Lol Mahamat Choua,zamani alikuwa mkuu wa serikali na kabla ya tukio la hivi majuzi alikuwa mkuu wa kamati inayotekeleza mabadiliko ya kidemokrasia.

Upande wa upinzani unasema Choua na wengine wawili walikamatwa na watu waliokuwa wamevaa sare za jeshi.

Kukamtwa kwao kulizua malalamiko kutoka jamii ya kimataifa hususan kundi la kutetea haki za binadamu-Amnesty International likisema linahofia maisha ya viongozi hao.

 • Tarehe 15.02.2008
 • Mwandishi Kalyango, Siraj
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo https://p.dw.com/p/D7wA
 • Tarehe 15.02.2008
 • Mwandishi Kalyango, Siraj
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo https://p.dw.com/p/D7wA
Matangazo

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com