Caracass: Rais wa Vernezuela, Hugo Chavez, anataka kutaifisha makampuni ya nishati na ya mawasiliano ya simu ya nchi yake. | Habari za Ulimwengu | DW | 09.01.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

Caracass: Rais wa Vernezuela, Hugo Chavez, anataka kutaifisha makampuni ya nishati na ya mawasiliano ya simu ya nchi yake.

Rais Hugo Chavez wa Venezuela anapanga kuliomba bunge la nchi yake limpe madaraka maalum ambayo yatamruhusu kupitisha sheria kwa amri yake. Katika hotuba yake ya televisheni alielezea mipango yake ya kujenga dola ya kijamaa na kuyataifisha makampuni ya nishati na mawasiliano ya simu. Rais Chavez ambaye alichaguliwa tena kuwa rais mwezi uliopita, alisema pia anapanga kuibadilisha katiba ya nchi ili kumaliza uhuru wa benki kuu ya nchi hiyo. Bwana Chavez ataapishwa kesho kuwa rais wa Venezuela kwa kipindi cha tatu.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com