Bush ziarani Mashariki ya Kati | NRS-Import | DW | 09.01.2008
 1. Inhalt
 2. Navigation
 3. Weitere Inhalte
 4. Metanavigation
 5. Suche
 6. Choose from 30 Languages

NRS-Import

Bush ziarani Mashariki ya Kati

Rais G.Bush wa marekani amewasili leo Mashariki ya kati kwa ziara ya siku 8.

default

Rais Bush na OlmertRais George Bush wa Marekani ana azma katika mwaka wake wa mwisho wa urais kusukuma mbele juhudi za amani za kuutatua mgogoro wa Mashariki ya kati.Kwa shabaha hiyo, amefunga leo safari ya siku 9 ya Mashariki ya Kati.Wachunguzi wanaona amekawia mno kufunga safari hiyo.


Rais George Bush kabla ya kuondoka Washington kuanza ziara ya hii alisema kwamba anaifurahia sana .


"Ninafurahi kwenda Mashariki ya kati.Miongoni mwa azma zangu ni kuusukuma mbele utaratibu wa amani. "


Katika ziara yake hii ya siku 8,rais george Bush amekusudia kufanya mengi.Lakini, amekawia kutanabahi kwamba ana mengi ya kutenda -ndio hisia za mabingwa wengi wa maswali ya Mashariki ya kati. Kwani, imemchukua Bush miaka 7 tangu kushika hatamu za urais  na ndio kwanza  sasa anatia mguu wake nchini Israel. Bingwa wa mashariki ya kati Bruce Riedel asema:


"Kiroja cha mambo ni kuwa rais Bush  amepitisha  miaka 7 sasa madarakani kabla  kumjia fikra ya kuzuru Israel."


Bruce Riedel ni bingwa wa maswali ya Mashariki ya kati kutoka Taasisi ya Brookings Institute mjini Washington.

Kwa jicho la Riedel,George Bush , aliesaliwa na mwaka tu Iklulu mjini Washington, ni mtu aliefungwa mikono yote 2 "Lame duck".


"Bush ni mmmoja kati ya marais wasio na uwezo wa kutenda lolote la maana kabisa katika historia ya Marekani,kwani hata makamo-wake  hataki kumrithi wadhifa wake."


Makamo-rais  Dick Cheney, anaona  hapahitaji kufanywa juhudi za kusaka amani Mashariki ya kati.Inatokana na shinikizo la waziri wa nje Dr.condoleeza Rice ndipo rais Bush amefunga safari yake hii ya leo .Ilianzia kwanza ule mkutano wa annapolis hapo Novemba mwaka jana  na sasa ziara hii ya siku 8 inafuatia.


Pale George Bush alipiingia ikulu (white House) hakutaka kujishughulisha na balaa hili la kutatanisha la Mashariki ya kati.

Ni muda mfupi kabla Julai 2000,mtangulizi wake  huko Ikulu, Bill Clinton alikwama huko Camp David katika kupatanisha mgogoro huu.

bingwa wa Taasisi ya Brooking kwa maswali ya Mashariki ya kati Riedel anakumbusha Bill Clinton alikwishafanya juhudi za miaka 5 wakati George Bush amebakiwa na mwaka tu.Kuufumbia macho mzozo huu kumechangia kuchafuka kwa hali ya mambo tangu nchini Israel hata  katika ardhi ziliopo chini ya Mamlaka ya ndani ya wapalestina.

Sasa ikiwa ana uwezo sasa wa kuusukuma  mbele utaratibu wa amani au la ,Riedel anaona nio vyema kuwa hatahiv yo, george Bush amefunga safari hii kwenda Mashariki ya kati.Kwani, anaona hii pekee ni hatua barabara.


Anasema  kwamba,iwapo mgogoro huu ukiachiwa  pande zinazogombana kuutatua wenyewe,basi utazorota tu na mwishoe  utachafuka zaidi.uongozi wa Marekani katika kusaka ufumbuzi wake  ni muhimu sana-asema Riedel.

Kwani , miaka ya nyuma imebainisha kuwa bila ya Marekani mgogoro wa mashariki ya kati ni kitandawili kisichoweza kupatiwa ufumbuzi.

 • Tarehe 09.01.2008
 • Mwandishi Engelke, Anna / Jerusalem (NDR) NEU
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo https://p.dw.com/p/CmvC
 • Tarehe 09.01.2008
 • Mwandishi Engelke, Anna / Jerusalem (NDR) NEU
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo https://p.dw.com/p/CmvC

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com